Dodoso la tathmini ya utekelezaji wa sera ya taifa ya vijana (2007)

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ikishirikiana na Economic and Social Research Foundation wanakusanya taarifa muhimu kutoka kwa vijana na wadau wa maendeleo ya vijana ili kuona kama malengo na matamko ya Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 yamefikiwa kwa kipindi cha miaka 8 ya utekelezaji wa Sera hii. Taarifa zitakazopatikana zitakuwa ni siri na zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Sehemu ya Kwanza: Taarifa Binafsi za Wahojiwa

Q1. Jina la Taasisi/Asasi/unayofanyia


Q2. Kundi ulipo - Chagua

Mzee Mtu wa Makamu Kijana Mtoto Nyingine

Q3. Jinsia (Tafadhali Chagua)    Mwanaume Mwanamke

Q4.Umri -

Q5. Kiwango chako cha elimu -

Q6. Je uelewa wa wananchi juu ya Sera ya Maendeleo ya Vijana upo je?.

 

Sehemu ya Pili: Athari za Kuwepo kwa Sera


Q7. Je kuna ongezeko lolote la Vijana wanaopata ajira kupitia mikakati sera hiyo?

Q8. Vipi kuhusu matamko ya Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, Je yanatosheleza?

Q9. Vipi kuhusu Dira ya Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, Je inatosheleza?


Q9b. Kama hapana toa ushauri

Q10. Vipi Dhamira ya Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, Je inatosheleza?

Q11. Je changamoto zipi kubwa zinazokwamisha ushiriki wa vijana katika maendeleo? Taja changamoto tano (5)

1-
2-
3-
4-
5-

Q12. Je kuna sera zozote zilizodurusiwa zilizokuwa zinaathiri utendaji wa Sekta ya Vijana ?.

Q13. Je kuna sheria zozote zilizodurusiwa zilizokuwa zinaathiri utendaji wa Sekta ya Vijana ?.

Q16. Je Maendeleo ya sayansi na Teknolojia yameongeza uelewa wa Jamii na hususan Vijana?

Q17. (a) Je kumekuwa na ongezeko lolote la ajira kwa vijana kupitia mikakati
mbalimbali iliyowekwa na serikali?

Q22. Je kwa mtizamo wako tatizo la ajira linaikumba zaidi jinsi gani katika jamii?

Q23. Je kwa mtizamo wako tatizo la ajira linaikumba zaidi watu wa umri gani katika jamii?

Q24. Je kuna mipango yeyote ambayo imeandaliwa ya kuhamasisha ajira kwa vijana katika jamii?

Q25. Je maeneo gani ya kipaumbele ambayo unafikiri yataongeza nafasi za ajira kwa vijana?

Q26. Je makundi gani ya vijana ambayo unafikiri hawakushirikishwa kikamilifu katika masuala ya maendeleo yao?

Q27. Vipi kuhusu utayari wa vijana katika shughuli kujitolea?

Sehemu ya Tatu: Taarifa ya Taasisi Zinazosimamia Sekta

Q29 Je unaridhishwa na utendaji na mchango unaotolewa na taasisi/asasi na wadau wanaosimamia Sekta ya Vijana?

Q30. Nini kifanyike kuwezesha taasisi/asasi na wadau muhimu wa Sekta ya Vijana na majukumu yao ili kuendeleza Sekta husika?
1-
2-
3-

Sehemu ya Nne: Ushauri/Maoni ya Jumla
Q31. Nini kifanyike ili kuweza kuboresha na kuendeleza Sekta ya Maendeleo ya Vijana nchini;

1-
2-
3-


admin