Home About Us Send Us Docs Tell a Friend Public Info Contact Us  
    Search Information:
Advance Search  
 
 
Tanzania Online News and Highlights


 
News Archive   
Search by Category: Search by Sub Category: Search by Keyword
Show All » Business & Economy » Tourism »

Share |

Hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii 2009/2010 -Mh. Shamsa Mwangunga (MB.) - July-13-09

UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja kwamba kutokana na taarifa iliyowasilishwa leo ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji kwa mwaka 2008/2009 na Mwelekeo wa Kazi kwa mwaka 2009/2010. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya fedha kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2009/2010. 2. Mheshimiwa Spika, Napenda kuishukuru kwa dhati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kwa kujadili makadirio ya matumizi ya fedha kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2009/2010. Wizara yangu itazingatia na kutekeleza mapendekezo ya Kamati hiyo, pamoja na yale yatakayotolewa na Waheshimiwa Wabunge wakati wa kujadili hoja hii.

Full Text


« Go Back


 
Copyright © 2001 - 2008 Tanzania Online - funded by JP4 Program and Tanzanian Government and hosted by ESRF