Home About Us Send Us Docs Tell a Friend Public Info Contact Us  
    Search Information:
Advance Search  
 
 
Tanzania Online News and Highlights


 
News Archive   
Search by Category: Search by Sub Category: Search by Keyword
Show All » Health » »

Share |

Mkakati wa Pili wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (2008 - 2012) - May-19-09

Kwa zaidi ya miaka ishirini, Tanzania imekuwa ikijitahidi kudhibiti janga la UKIMWI, ambalo linaendelea kuangamiza maelfu ya raia wake na kuathiri juhudi za maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Nchi inakabiliwa na maambukizo yaliyoenea nchi nzima kwa wastani wa ushamiri wa VVU wa asilimia 5.8. Uambukizo wa VVU unaenea miongoni mwa wananchi nchini kote, mijini na vijijini, huku kukiwa na tofauti za wazi kati ya mikoa na ndani ya mikoa. Madhara makubwa ya janga hili yapo katika sekta zote kwa sababu yanaleta mateso miongoni mwa watu binafsi, familia na jamii nchini kote. Idadi ya mayatima inaongezeka kila siku kadiri janga hili linavyowaua wazazi. VVU/UKIMWI vimeongezea taifa gharama juu ya uchumi wake ambao ni dhaifu.

Full Text


« Go Back


 
Copyright © 2001 - 2008 Tanzania Online - funded by JP4 Program and Tanzanian Government and hosted by ESRF